Kijana mmoja jijini New York, Marekani mwenye umri wa miaka 30, Michael Ratondo, ameamriwa na mahakama kuhama nyumbani kwao baada ya wazazi wake kumfungulia mashtaka.
Sehemu ya nakala ambazo wazazi wake waliwasilisha mahakamani zilikuwa zimeandikwa ''Kuna kazi zinapatikana hata kwa wale wenye historia mbaya ya kufanya kazi kama wewe'' ''Nenda katafute kazi-unapaswa kufanya kazi!''
Christina na Mark Rotondo walifungua shauri hilo wiki iliyopita baada
ya juhudi zao za kumuondo kijana wao nyumbani ikiwemo kumpa dola za
Marekani 1,100 na kumtaka auze baadhi ya vitu vyake ikiwemo gari yake
mbovu aina ya Volkswagen Passat kugonga mwamba.
Michael amekiri mahakamani kuwa hakuwahi kuchangia gharama zozote nyumbani, na kuwa alikula pesa aliyopewa ili ahame.
Kijana huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa atakata rufaa, na amepanga kuondoka nyunbani miezi mitatu ijayo.
(BBC)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni