
Baada ya kuwakosa watani zake wa jadi, Yanga, kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima inaelezwa tayari amesharejea nchini kujiunga na klabu yake.
Niyonzima
alisafiri wiki iliyopita kuelekea kwao Kigali, Rwanda kwa ajili ya
kuhudhuria msiba wa dada yake aliyefariki baada ya kuumwa.
Niyonzima amerejea huku Simba ikiwa na nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi, ambapo mpaka sasa imejikusanyia jumla ya alama 62.
Simba
inahitaji kushinda mechi moja pekee na kwenda sare ama suluhu katika
michezo ijayo ya ligi ili iweze kufikisha jumla ya alama 67 ambazo
hazitoweza kufikiwa na timu yoyote ile.
Kikosi
cha Simba kinaendelea na mazoezi yake katika Uwanja wa Bocco Veterani
kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC utakaofanyika
kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Jumapili ya wiki hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni