
Jumla ya Kaya 40 katika Kata ya Arusha chini wilayani Moshi vijijini hazina mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Kilimanjaro.
Eneo la Kata ya Arusha chini limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara kutokana na sababu za kijiografia.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ametembelea eneo lililoathiriwa na mvua na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya mvua hizo zinazoendela.
Mmoja wa
wakazi wa eneo, Juma Mussa mkazi wa Mikocheni lililoko ukanda wa
tambarare wa Mkoa wa Kilimanjaro ameomba serikali kuweka miundombinu
itakayowaondolea hofu ya mafuriko.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni