mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania
blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla
kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Jumamosi, 19 Mei 2018
Mwanafunzi afariki kwa mlipuko
Mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Sabasaba jijini
Mwanza, Dotto Baraka (13) amefariki dunia baada ya kulipukiwa na betri
ya simu aliyokuwa akiiunganisha na radio chakavu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha tukio hilo
ambapo amesema limetokea Mei 17, mtaa wa Igoma Mashariki jijini Mwanza.
“Baada ya kutoka shuleni, marehemu akiwa na watoto wenzake alianza
kutengeneza radio chakavu kwa kuchukua betri ya simu na kuunganisha
kwenye nyanya za radio hiyo akitumia mdomo ndipo mlipuko ulipotokea na
kusababisha kifo chake," amesema Kamanda Msangi.
Aidha Kamanda Msangi ameongeza kuwa wakati tukio hilo linatokea, wazazi
wa watoto hao walikuwa safarini huko wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Hata hivyo katika tukio hilo hakuna mtoto mwingine aliyejeruhiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni