

Mmiliki wa Mtandao wa Kijamii wa Facebook, Mark Zuckerberg kwa mara nyingine tena ameomba radhi wateja wote kwa madai kuwa kampuni yake haijawajibika vya kutosha kudhibiti baadhi ya mambo kama vile habari za uzushi katika mtandao huo, kuingilia chaguzi na taarifa binafsi za wateja wake kudukuliwa.
Zuckerberg ameomba radhi tena baada ya kuibuka taarifa za kuwasilisha utetezi wake.
Marck Zuckerberg amesema hayo mbele ya Bunge la Ulaya, wakati akieleza hatua ambazo Facebook imekuwa ikizichukua ambazo ni kuweka uhalali wa baadhi ya vitu ndani ya mtandao huo na kuhakikisha kuna mfumo unaolinda kudukuliwa kwa taarifa binafsi za wateja.
''Kwa sasa unapotumia mtandao wetu, utaongozwa na taarifa zako ili uweze kuingia na kupitia ukurasa wako na taarifa zake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni