Real Madrid walitinga hatua hiyo ya fainali baada ya kuwoandoa Juventus huku Liverpool wakitoa AS Roma ya Italy.
Kuelekea mechi hiyo, nyota wawili ndiyo wanaozungumziwa zaidi hivi sasa ni Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah wanaopewa nafasi kubwa ya kuzibeba timu zao.
Ronaldo amekuwa hana msimu mzuri nchini Spain na Madrid katika La Liga wakati huo nyota Mmisri, Salah amekuwa na mwaka mzuri kwa kutwaa tuzo kibao ikiwemo ya mchezaji bora nchini England msimu huu.
Mechi hii inayotarajiwa kuanza majira ya saa 3 na dakika 45 usiku inasubiriwa na wadau wengi wa michezo duniani ambao wana shauku kubwa ya kuona nani atalibeba taji hilo kubwa duniani.

Bado saa kadhaa tuweze kushuhudia fainali ya UEFA Champions League
inayozikutanisha timu za Real Madrid ya Hispania dhidi ya Liverpool ya
England ambapo wanacheza mchezo huo wa fainali Kyiv nchini Ukranine
katika uwanja wa wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 70000.
1- Real Madrid na Liverpool wamekutana mara 4 toka February 25 2009, Real Madrid akifanikiwa kushinda mara mbili katika michezo ya hatua ya makundi wakati Liverpool na akiifunga Real Madrid mara mbili katika michezo ya hatua ya 16 bora February 25 2009 na March 10 2009.
2- Kingine cha kuvutia ni kuhusiana na kauli kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania na club ya Real Madrid Vicente del Bosque ambaye amesema hakuna mchezaji hata mmoja wa Liverpool unaeweza kumlinganisha na mchezaji wa Real Madrid.
3- Wachezaji Mohamed Salah wa Liverpool na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ndio vivutio zaidi na kila mmoja anatamani kuona ni mchezaji gai atafanya maajabu zaidi ya mwenzake usiku wa leo, Ronaldo na Salah wote wamefunga jumla ya magoli 44 msimu huu ila Salah amecheza mechi nyingi zaidi ya Ronaldo.
4- Staa wa Liverpool Mohamed Salah ambaye ni muumini wa dini ya kiislamu licha ya kuwa na msimamo wa dini yake lakini leo ameridhia kutofunga Ramadhani kutokana na mchezo huo.
5- Kama Real Madrid watachukua Kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo leo kocha wao Zinedine Zidane ndio atakuwa kocha wa kwanza kuwahi kutwaa taji la UEFA Champions League mara tatu mfululizo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni