FAINALI ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2018 inafanyika leo Olimpiki
NSK mjini Kiev, Ukraine ikizikutanisha Liverpool ya England na Real
Madrid ya Hispania kuanzia Saa 21:45 usiku.
Hiyo itakuwa fainali ya 63 ya michuano hiyo inayoandaliwa Shirikisho la
Soka Ulaya (UEFA), na msimu wa 26 tangu ipewe jina jipya la Ligi ya
Mabingwa Ulaya kutoka lile la zamani la Klabu Bingwa Ulaya.
Mshindi wa mchezo wa leo atakutana na mshindi wa fainali ya UEFA Europa
2018 katika Super Cup ya UEFA. Pia watafuzu kuanzia hatua ya Nusu
Fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA mwaka 2018 FIFA kama
wawakilisji wa UEFA
Mabingwa watetezi, Real Madrid walitinga fainali ya 16 ya rekodi baada
ya ushindi wa 4–3 jumla dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani wakiwatupa
mashindanoni kwa mara ya pili mfululizo.
Na hii ni fainali ya tatu mfululizo ya Real Madrid na fainali ya nne
kwenye mashindano matano huku ikipewa nafasi ya kushinda taji la 13 la
rekodi, baada ya awali kushinda katika miaka ya 1956, 1957, 1958, 1959,
1960, 1966, 1998, 2000, 2002, 2014, 2016 na 2017; na kufungwa katika
fainali za 1962, 1964 na 1981.
Liverpool wameingia fainali ya nane, na ya kwanza tangu mwaka 2007,
ambayo walishinda kwa jumla ya mabao 7–6 dhidi ya Roma ya Italia.
Wameshinda taji hilo mara tano katika miaka ya 1977, 1978, 1981, 1984 na
2005, na wamefungwa mara mbili kwenye fainali 1985 na 2007.
Mwandishi mmoja aliyehudhuria mazoezi ya Real Madrid jana aligongwa
usoni na mpira uliopigwa na Cristiano Ronaldo na kuchanika kidogo jirani
ya jicho.
Real walikuwa wanafanya mazoezi Uwanja wa Olimpiki mjini Kiev kuelekea
fainali leo na ndipo Ronaldo alipompiga na mpira mwandishi huyo. Lakini
Ronaldo alimuomba msamaha kwa ishara ya mkono mwandisi huyo aliyepatiwa
huduma ya kwanza uwanjani hapo.
Beki ghali aliyesajiliwa Liverpool kwa dau la Pauni Milioni 75 amesema
kwamba Real Madrid hawajawahi kukutana na timu kama yao kabla.
Amesema; nani anajali? Alipoulizwa kama Wekundu hao walistahiloi kufika gainali ya Ligi ya Mabinghwa Ulaya.
Mashabiki wa Liverpool walishambuliwa na wababe mjini Kiev juzi, kabla ya Polisi kuthibitisha watu wawili walikamatwa.
Picha za kutisha zimeonyesha watu wakishambuliana kwa kwa magongo, meza
na viti. Polisi wa Merseyside wamesema wana taarifa za tukio hilo na
wana Maofisa wao mjini Kiev.
Gwiji wa England, David Beckham amemtaka mchezaji mwenzake wa zamani wa
Real Madrid, Zinedine Zidane sasa kocha wa klanbu hiyo kushinda fainali
ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool: 'Tafadhali wafunge
Liverpool'
Beckham ni mpenzi wa Manchester United ambao ni wapinzani wa Liverpool.
Beckham aliondoka Old Trafford kuhamia Los Blancos kwa dau la Pauni
Milioni 25 mwaka 2003.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni