Serikali ya China imetoa Msaada wa Sh. Bilioni 146.47 za Kitanzania , madhumuni makubwa ya msaada huo yanalenga kukijenga upya chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuwa Chuo Kikuu cha Usafirishaji Tanzania ambacho kipo Mabibo jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Vyombo vya habari, Katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango, Bw. Doto James amesemaSerikali ya China baada ya kuona mara nyingi tunaiomba itusaidie kujenga reli ya Kati kwa kiwango cha Standard Gauge, imetoa msaada kuisaidia ujenzi wa vipande vya reli vilivyobakia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni