
Wanawake walio na hasira
wameandamana leo mjini Nairobi kulalamika tuhuma za kufukuzwa kwa
mwanamke mmoja kutoka mgahawa mmoja kwa kumyonyesha mtoto wake.
Wanawake
hao wameelekea katika mgahawa wa Olive Restaurant, ambako mama huyo
anatuhumu kuwa aliambiwa ajifunike wakati anamnyonyesha mtoto wake
mwenye mri wa mwaka mmoja.
Alieleza kisa kilichompata katika kundi moja la akina mama katika mtandao wa kijamii Facebook, na kusema kuwa aliambiwa akamyonyeshe mtoto wake chooni, jambo lililomuacha akihisi kudharauliwa.
Mgahawa huo umeomba utulivu udumishwe kufutia ghadhabu hiyo kubwa ya wanawake nchini ukiomba kupewa muda kulishughulikia suala hilo kwa ndani.
Mojawapo ya mashirika yalioshiriki maandamano hayo leo ni Muungano wa mawakili wanawake FIDA.

Mswada wa afya nchini wa mwaka 2017 unaeleza kuwa waajiri wote nchini wanastahili kutenga nafasi kuwaruhusu wanawake kuwanyonyesha watoto wao katika maeneo ya kazi.
bbc swahili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni