Msanii
wa maigiizo nchini Wastara Juma amefunguka na kuongelea yaliyokuwa
yanajiri alipokuwa hospitali na kusema kuwa kipindi yupo katika matibabu
yake nchini india , mwanaharakati Mange kimambi aliwapigia simu
madaktari na kuwadanganya kuwa ni dada wa Wastara na kutaka kujua
details zake.
Wastara alisema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha kikaangooni live kinachorushwa na EATV, Ambae alizusha uongo mwingi kuhusu matibabu ya msanii huyo baada ya kuonekana kwa cannula ambae ilisemekana kuwa imegeuzwa kwa mujibu wa Mange ingawa Wastara mwenyewe alikataa swala hilo.
"Mange
kimambi aliwahoji madaktari nikiwa india,mimi nikashaanga kuona
madaktari wanakuja wananiuliza mimi ni nani Tanzania, nikawajibu mimi ni
msanii ....wakaniuliza kama ninamfahamu huyu mtu anaitwa Mange Kimambi
anasema kuwa ni dada yangu, na pa ni mwamndishi wa habari
anakuulizia, nikawajibu sina dada mwenye cheti cha milembe."
Wastara
anasema kuwa kama mange kimambi angekuwa na akili basi alitakiwa
kuangalia ile cannula vizuri kabla ya kuanza kuweka maneno katika
mitandao kuhusu kudanganya
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni