Mama
mzazi wa aliyekuwa msanii wa Bongo movie Marehemu Steven Kanumba, Mama
Kanumba ameibuka na jipya tena huku safari hii akisema anatamani kwenda
jela kumuona Lulu.
Mama
Kanumba hakuwa na uhusiano mzuri na Lulu kwani mpaka a nafungiwa
walikuwa kama wana ugomvi fulani huku Mama Kanumba alidai sababu kubwa
ni Lulu kumtupa mama huyo na kutomjali kwa lolote.
Miezi
michache iliyopita Muigizaji wa Bongo movie Lulu Michael alifungwa
gerezani kwa miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila
kukusudia aliyekuwa mpenzi wake Steven Kanumba.
Baada
ya Lulu kufungwa Mama Kanumba hakusita kuonyesha furaha yake juu ya
Lulu kufungwa na baadae alipoulizwa endapo ana mpango wa kwenda
kumtembelea Lulu gerezani alisema hajui mpaka afanye mazungumzo na Mungu
wake.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Mwananchi Communications, Mama Kanumba ameibuka na kusema anatamani kwenda kumuona Lulu jela:
"Tangu
Lulu kahukumiwa nimekuwa nikipokea lawama na watu kunitusi kuwa mimi
ndio sababu, na kusahau ya kwamba mimi nilishamsamehe kama binadamu na
siye niliokuwa mlamlamikaji katika kesi hiyo isipokuwa alishitakiwa na
serikali”.
Lakini
Mama Kanumba amesisitiza kuwa yote yaliyotokea anamuachia Mwenyezi
Mungu kwani yeye kufungwa hakuwezi kumrudishia mtoto wake ambaye
amekwisha tangulia mbele ya hali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni