Ijumaa, 9 Machi 2018

TCRA MKO WAPI KWA MATUSI HAYA MAZITO YANAYOTUKANWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII?

Na deus liganga
nianze  makala  yangu kwakulipongeza jeshi la polisi visiwani zanzibar kwakutoa taahadhari kwa watamiaji wa  mitandao  ya kijamii ambao wanatumia mitandao hiyo, kwa kuwatukana  viongozi na watumiaji wenzao kwani endapo watakamatwa hatua za kisheria  zitachukuliwa dhidi yao.
nimeanza na pongezi kwa serikali ya zanzibar kwasababu wameonyesha uthubutu katika jambo hili, na wala sina maana kuwa jeshi la polisi Tanzania bara halifanyi kazi .

Ni ukweli usiopingika  suala la maadili miongoni mwa watumiajiwengi wa  mitandao ya kijamii  ni kizungumkuti haswa kwasasa kumekuwa na kurasa mbalimbali ,makundi, maarufu kama pages katika mitandao kama vile, facebook,instagram,whatsapp ,na mengine mingi wamekuwa wakitukana matusi ya nguoni wenzao pasi na kificho.

wimbil lingine la watukanaji lipo katika kurasa za michezo ''pages''na yale makundi ya  wanachama wa kisiasa katika mitandao hiyo ambapo wa mashabiki wa timu za mpira hutukanana matusi mazito ya nguoni ambapo kwangu inakuwa vigumu kuyaandika ,sambamba na wanachama na wanazi wa vyama vya siasa, ,pamoja timu za wasanii muziki wa kizazi kipya.
najaribu kujiuliza  hivi mamlaka husika havioni vitendo hivyo?mpo wapi mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA? jeshi la polisi lipo wapi?sheria ya makosa ya mitandao ya kijamii ya mwaka 2015 ina fanya nini? ilitungwa ili ifanye nini? waziri wa mamlaka husika yupo wapi?
hakika ni maswali mengi juu ya hali hii. tunapokwenda sio pazuri hata kidogo,kwasasa mtu kumtukana mwenzie ni jambo la kawaida ,watu wanachapisha  matusi ya nguoni ,katika mitandao hiyo

imefikia kipindi baadhi ya watanzania wenzetu hawawezi kuchangia mada yeyote bila kutia tusi  au lugha ya maudhi kwa mwenzake , tunakwenda wapi?
wanajifunza nini watoto ambao kulingana na ulimwengu unavyokwenda sasa na wao wamejikuta ndani ya mitandao hii, ambao wengi wao ni wanafunzi , tunategemea nini?

kulingana na vyanzo mbalimbali,  tangu kuanzishwa kwa sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015 kumewezesha jeshi la polisi nchini kufuatilia kwa karibu nakushighulikia uhalifu mitandaoni ambapo kwa kipindi cha mwezi januari hadi  mwezi juni mwaka 2017 jeshi la polisi limeweza  kukamata watuhumiwa315 kufikisha mahakamani kesi 153,kesi 19 zilipatikana na hatia na zingine zipo chini ya upelelezi, lakini licha ya juhudi hizo bado wimbi la suala hili linakuja kwa kasi.

na kulingana na utafiti uliofanywa mwaka jana ,2017 lugha ya matusi imeendeleea kutumika huku mkoa  wa Dar es salaaam ukishika nafasi ya kwanzana mkoa wa mwanza kuongoza kwa  upande wa makosa ya wizi wa fedha mtandaoni.

kuna haja kwa viongozi wetu wa mamlaka husika  kuchukua hatua za haraka kuhusu matusi na lugha za kuudhi katika mitandao ya kijamii vinavyoendelea kushamiri katika nchi yetu.
ni vyema TCRAna jeshi la polisi , na mawaziri husika kuliona hili mapema  hali sio nzuri .


ushabiki wa timuza mpira wa miguu bila matusi inawezekana
ushabiki wa timu za muziki bila matusi inawezekana
kuchapisha  ujumbe bila kutukana inawezekana
tumia vyema mitandao ya kijamii kwa manufaa ya umma, 
mungu ibariki Tanzania
makala hii imeandikwa na Deus liganga mwanahabari 
0659944423
mzeeliganga@gmail.com








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni