Jumanne, 6 Machi 2018

RIPOTI: Tanzania yapanda nafasi 13 duniani mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi



 serikali imesema ripoti iliyotolewa shirika la kimataifa linaloangalia hali ya Rushwa na mapambano dhidi ya ufisadi duniani imeeleza katika kipindi cha mwaka mmoja Tanzania imepanda nafasi 13 duniani imesogea kutoka chini kwenda juu.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dkt. Hassan Abbas Mjini Dodoma alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa miradi na ahadi mbalimbali za Serikali.
“Kwa kipindi kifupi mpaka kufikia mwezi Februari moja ya mambo makubwa ambayo yamejitokeza ni ripoti ya Transparency International hili ni shirika la kimataifa linaloangalia hali ya Rushwa na mapambano dhidi ya ufisadi duniani sasa tu nipende kusisitizi ani ripoti ambayo mnaifahamu ilitolewa mwezi Februari tarehe 21 mwaka huu na hii ripoti kimsingi sisi kama Tanzania fahari yetu kama nchi ni kwamba mapambano ambayo Mh. Dkt. John Pombe Magufuli na timu yake na Watanzania kwa ujumla tumeamua kuyashikia bango ya kupambana na rushwa na ufisadi yameanza kulipa kwa mujibu wa ripoti hii Tanzania imepanda nafasi 13 duniani yaani imesogea kutoka chini inakuja juu na nafasi hizo 13 ni katika kipindi cha mwaka 1,“ alisema Dkt. Abbas.
“Kwahiyo juhudi zilizofanyika kwa mwaka 2016 tu kuja 2017 tayari nchi yetu kwa mujibu wa hii Taasisi na ripoti yao inaitwa corruption Perception Index 2017 ni ripoti ya mwaka 2017 ikiangalia jitihada na juhudi ambazo zimechukuliwa na nchi mbalimbali katika dunia nzima kwahiyo tumepanda kwa nafasi ya 13 kwa mafanikio ya mwaka mmoja tunaamini ikija ripoti ya 2017 /2018 nchi yetu itaendelea kupanda kwsababu ya dhamira yetu iliywazi katika kupambana na rushwa.“

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni