Kwa upande wa Township Rollers kesho watacheza na Yanga uwanja wa Taifa baada ya kuwatoa El Merreikh ya Sudan katika round ya awali, hivyo kuelekea mchezo huo, hivyo kuelekea mchezo huo Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa ameongea na waandishi wa habari na kueleza kuwa Township Rollers sio timu ya kubeza.
“Kikubwa hasa ni kuwajulisha watanzania kuhusiana na mchezo wetu wa CAF Champions League, sisi tuna mechi kesho na tumuombe Mungu atusaidie ili tuweke mazingira ya kuingia katika makundi, hii sio timu ya kuibeza ipo vizuri kiuchumi na imeitoa El Merreikh ambao huwa wanafanya vizuri Champions League” Mkwasa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni