Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya
iliendelea tena usiku wa jana ambapo mechi iliyokuwa inasubiriwa kwa
hamu na mashabiki wa soka Afrika na duniani wa ujumla kati ya FC.
Barcelona dhidi ya Chelsea kumalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa
mabao 3-0.
Alikuwa ni Messi aliyeanza kucheka na nyavu dakika ya mapema
zaidi, dakika ya 3 na baadaye Oeusman Dembele akafunga la pili dakika
ya 20, kabla ya Messi kuongeza jingine la 3 kwenye dakika ya 63 kipindi
cha pili.Barcelona sasa inasonga mbele kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya mechi ya awali kwenda sare ya 1-1 pale Stamford Biridge.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni