Alhamisi, 15 Machi 2018

DIAMOND PLATNUMZ KUZINDUA ‘A BOY FROM TANDALE’ NCHINI KENYA

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz (katikati) wakati akiongea na wanahabari leo nchini Kenya kuelekea uzinduzi wa albamu yake ya ‘A boy from Tandale’ akiwa na mkali wa RnB kutoka nchini Marekani, Omarion (kulia).

Wakiendelea kuwasikiliza wana habari.

Diamond Platnumz akiongea na mkali wa RnB kutoka nchini Marekani, Omarion (kulia).
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameongea na wanahabari sababu iliyomsukuma kwenda nchini Kenya kuzindua album yake ya ‘A boy from Tandale’ badala ya kuzindulia hapa Tanzania kama wasanii wengine wanavyofanya.
Diamond Platnumz amesema sababu kubwa iliyofanya azindulie Kenya album yake ya ‘A boy from Tandale’ ni kuimarisha mshikamano wetu kati ya Tanzania na Kenya kama ndugu tena kwa vitendo na sio kwa maneno kama baadhi ya watu wanavyoongea.
Hata hivyo, Jumatano  hii Machi 14, 2018 kutakuwa na Listen Party ya album ya ‘A boy from Tandale’ ambapo kwa mara ya kwanza mashabiki na wadau wa muziki Tanzania watapata nafasi ya kusikiliza album hiyo inayosubiriwa kwa hamu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni