Inaelezwa kuwa gari yake ndogo aliyokuwa akiitumia aina ya Toyota LandCruiser lilikutwa limechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyoko mkoani Mara siku ya jana lakini yeye mwenyewe bado hajapatikana.
Kwa mujibu wa familia ya Bwana Josiah, ambayo inaishi mkoani Mwanza, siku ya kupotea kwa Josiah ambayo ni February 27, majira ya usiku, Josiah alimpigia simu mkewe na kumwambia kuwa atarudi nyumbani na mgeni, na hayo yakawa mawasiliano yao ya mwisho hadi leo.
Japokuwa gari hilo limepatikana, yeye mwenyewe hajapatikana hivyo hakuna ushahidi unaoonesha kuwa amechomwa akiwa ndani ya gari hilo au la, na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.
Mabasi ya Super Sami yanafanya safari zake kuanzia mkoa wa Mwanza, kwenda mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa pamoja na Kagera.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni