FA walimpa muda wa kujitetea Pep Guardiola kutokana na kitendo chake cha kupenda kuvaa ribbon ya njano mara kwa mara katika game za Ligi Kuu England, nembo ambayo inahusishwa na masuala ya kisiasa nchini Hispania.
Hivyo FA leo imetangaza kumpa onyo kali na kumpiga faini ya pound 20,000 (Tsh milioni 62.4) kwa kosa hilo lakini Kama utakuwa unakumbuka vizuri Pep Guardiola amekuwa akivaa nembo hiyo ambayo inatumika na kutafsirika nchini kwao Hispania na watu wanaodai uhuru wa jimbo la Catalunya kujitenga na Hispania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni