Serikali kupitia Wizara ya Afya imezitambua rasmi aina ya dawa tano
za asili baada ya kuzikagua na kujiridhisha kuwa zinatibu matatizo ya
nguvu za kiume.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile
Amezitaja dawa hizo leo Machi 13, 2018, Msajili wa Baraza la Tiba za
Asili na Mbadala, Dkt. Ruth Suza katika mkutano na waandishi wa habari
amesema ni Ujana, Sudhi, Vatari, IH Moon na Coloidal Silver.
Dkt. Suza amesema mpaka serikali kukubali dawa hizo kutumika,
walitumia kitengo cha Boring cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa
kushirikiana na Mkemia Mkuu wa Serikali.
Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile
ametoa agizo kwa waganga wote wa tiba asili na tiba mbadala kuacha mara
moja kutoa matangazo yao mbalimbali kupitia vyombo vya habari na mabango
ya barabarani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni