Watu 28 wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA
wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na
kosa la kufanya mkusanyiko usiokuwa halali katika Barabara ya Kawawa
maeneo ya Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam.
Washtakiwa hao wamesomewa kosa hilo na Wakili wa serikali, Faraji Nguka mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa.
Wakili Faraji Nguka, amedai kosa hilo wamelitenda February 16, 2018 barabara ya Kawawa maeneo ya Kinondoni Mkwajuni ambapo walifanya mkusanyiko usio halali wakiwa na nia ya kusababisha uvunjifu wa amani.
Baada ya kusomewa kosa hilo washtakiwa walikana ambapo Wakili Nguka ameeleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Hata hivyo, Hakimu Mwambapa alitoa masharti ya dhamana kwa washtakiwa ambapo wametakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini Bondi ya Sh.Milioni moja na nusu, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi March 8, 2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (PH).

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni