
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa vyama vya ushirika waliokula fedha za wakulima wa korosho wilayani Masasi kuzirudisha na wakishindwa kufanya hivyo mali zao zikiwemo nyumba zitauzwa ili kufidia.
Waziri mkuu pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa kuhakikisha anawasaka viongozi wa chama cha ushirika cha msingi cha Nanyindwa wilayani Masasi ambao wamekula fedha za wakulima na kisha kutoroka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni