
jeshi la Polisi katika Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya linashikilia watu wawili ambao ni waganga wa Jadi kwa tuhuma za kumuunguza mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Emiliana Thomas mkazi wa Kijiji cha Omuga Wilaya ya Rorya mkoani humo kwa madai ya kumtibu mwanamke huyo kutokana na kuahidiwa kupata ujauzito.
Kamanda wa Polisi katika Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya, Henry Mwaibambe amewataja watuhumiwa hao kuwa Juma Ayoub na Michael Jacob wote wakazi wa Rorya.
Kwa mujibu wa Kamanda Mwaibambe, waganga hao walilenga kumchoma moto kuku ambaye alimwagiwa mafuta ya taa kwa lengo la kuondoka na mapepo yaliyodaiwa kumzuia mwanamke huyo kushika mimba na kumbe kwa bahati mbaya mafuta hayo pia yalimwagikia mwanamke huyo.
Mwanamke huyo amelazwa katika Hospitali yab Kowaki akiwa na majeraha ya kutisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni