Jumanne, 27 Februari 2018

UCHACHE WA MAHAKAMA:



Jaji mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma amesema ukosefu wa Mahakama Kuu katika mikoa 13 kati ya 31 nchini unakwamisha upatikanaji wa haki nyingi za wananchi hususan wale wa hali ya chini kiuchumi.
Ametolea mfano Mkoa wa Kigoma ambapo wananchi hulazimika kutembea zaidi ya kilomita 400 hadi Tabora ilipo Mahakama Kuu baada ya rufaa mkoani Kigoma ambapo wananchi wengi hushindwa kumudu gharama za usafiri, chakula na malazi na hivyo hukata tamaa na kupoteza haki zao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni