
Kipute cha Ligi Kuu Tanzania Bara kinataraji kuendelea tena Jumatano ya kesho kwa mchezo mmoja kupigwa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, ambapo Ndanda itaikabili Yanga.
Kuelekea mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Ndanda, Mussa Mbaya, amewatambia Yanga kuwa kesho ni lazima waache alama 3 mkoani Mtwara.
Mbaya
amesema anatambua kuwa Yanga wanafukuzana na Simba kuwania ubingwa wa
Ligi, lakini wanachokiangalia wao ni ushindi pekee kwenye mchezo huo.
"Sisi
tumejiandaa vema, na nawaambia mashabiki wetu wajiandae kupokea alama
tatu muhimu, ushindi utakuwa kwetu bila shaka yoyote" amesema Mbaya.
Ndanda
itakuwa mwenyeji wa pambano hilo ikicheza mchezo wa 19 sawa na Yanga,
lakini utofauti upo katika msimamo ambapo Ndanda ina alama 18, nafasi ya
13 na Yanga 37, nafasi ya pili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni