
Sridevi Kapoor
Sridevi amekuwa kwenye tasnia ya filamu kwa miongo minne ambapo amefanikiwa kushiriki kwenye filamu 300 na baadhi ya filamu zilizompa umaarufu ni kama Mr. India, Chandni, ChaalBaaz na Sadma.
Sridevi alitajwa kuwa mmoja wa wasanii wachache wa kike waliopata mafanikio makubwa bila ya msaada wa wanaume.
Baada ya taarifa hizo, maelfu ya watu walikusanyika nje ya nyumba yake jijini Mumbai huku waigizaji wenzake na viongozi wa serikalini akiwemo Rais wa India Ram Nath Kovind kupitia ukurasa wake wa Twitter akiandika “Shocked to hear of passing of movie star Sridevi. She has left millions of fans heartbroken. Her performances in films such as ‘Moondram Pirai’, ‘Lamhe’ and ‘English Vinglish’ remain an inspiration for other actors. My condolences to her family and close associates,”
Naye Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ameandika katika mtandao wa twitter “Saddened by the untimely demise of noted actor Sridevi. She was a veteran of the film industry, whose long career included diverse roles and memorable performances. My thoughts are with her family and admirers in this hour of grief. May her soul rest in peace.”
Kifo cha Sridevi kinakuja ikiwa ni miezi miwili imepita tangu mjomba wake ambaye alikuwa ni moja ya waigizaji nguli wa filamu nchini humo, Shashi Kapoor aage dunia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni