Hatahivyo habari kutoka Msumbiji, mvua zilizonyesha siku za hivi karibuni katika Mji wa Maputo zimesababisha rundo la takataka kuanguka na kuwafukia watu 17 ardhini hadi kupoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa.
Inaelezwa kuwa rundo hilo la takataka ambalo lilikuwa la mita 15 limefunika watu pamoja na nyumba saba.
Kwa mujibu wa Kiongozi wa Manispaa ya Ka Mavota, Despedida Rita amewaeleza waandishi wa habari kuwa miili 17 tu ndio iliyopatikana, lakini wana wasiwasi kuwa kuna uwezekano ipo miili mingine imefunikwa na hivyo jitihada za kuitafuta zinaendelea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni