Takribani
mwezi mmoja umepita, marubani wawili raia wa Kenya walitekwa na kikundi
cha waasi wa nchini Sudani baada ya ndege yao kupata ajali na jitihada
za kuwaokoa zilikuwa ziliendelea.
Habari njema leo February 20, 2018
ni kwamba marubani hao wameachiwa na waasi hao na kwa mujibu wa msemaji
wa waasi hao marubani hao wameachiwa baada ya kampuni ya bima kulipa
zaidi ya dola za Marekani 100,000 sawa na Tsh Milioni 24o za Kitanzania.
Fedha hii ilikuwa niyakulipa fidia ya kifo cha mtu mmoja aliyepoteza maisha baada ya ndege hiyo kupata ajali.
Marubani
hao Kapteni Pius Frank Njoroge na Msaidizi wa Rubani Kennedy Shamalla
wameripotiwa kuwasili salama mjini Juba na watarudishwa Kenya baadaye.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni