Wakati kikosi cha Simba kimekwea pipa
kwenda Djibouti kuivaa Gendamarie katika mechi ya Kombe la Shirikisho,
kiungo wake, Said Hamis Ndemla amekuwa kivutio kwa mashabiki wa soka
waliokuwa eneo hilo.
Ndemla alionekana kuchangamkiwa na
mashabiki wengi wakimuita jina lake na baada ya hapo wakaanza kujadili
suala la yeye kuwa na uwezo mkubwa wa kupiga mashuti wakati ana umbo
dogo.
"Anaonekana ni mdogo, lakini mikwaju yake hatari sana yule mtu aisee," alisema mmoja wa mashabiki na kuungwa mkono na wenzake.
Ndemla amekuwa na sifa ya kupiga mashuti
makali kiasi cha kujijengea imani hata ya kupata namba katika kikosi
chini ya Mfaransa, Pierre Lechantre.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni