Habari za muda huu kutoka nchini humo ni kwamba Bunge limemteua aliyekuwa Makamu Mkuu wa Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa kuwa Rais mpya wa Afrika Kusini na kueleza kuwa ndiye atakuwa kiongozi bora katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini humo.
Zuma alikuwa akikabiliwa na tuhuma nyingi, moja ikiwa ni kumhusisha na vitendo vya rushwa japokuwa mwenyewe amekanusha kuhusishwa na tuhuma hizo. Kutokana na hilo bunge lilipiga kura ya kutokuwa na imani naye na baadaye chama tawala ANC kikamlazimisha kuachia madaraka kwa hiari.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni