Jumatatu, 5 Februari 2018

Polisi walivyomchukua Diwani wa CHADEMA Arusha


Leo February 5, 2018 baadhi ya Madiwani wa CHADEMA katika Halmashauri ya Jiji la Arusha wamesusia na kutoka nje ya ukumbi wa Halmashauri wakati wa kuapishwa kwa Madiwani Wapya wawili waliochaguliwa kupitia Chama cha Mapinduzi kwa madai ya kupinga walivyochaguliwa.
Baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza la Madiwani, Jeshi la Polisi Arusha limemshikilia Diwani wa Kata ya Daraja Mbili Prosper Msofe kwa madai ya kukutwa na Nyaraka za siri za serikali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni