Kaka wa marehemu, Moi Kiyeyeu amesema baada ya kuaga mwili huyo siku ya Alhamisi, atazikwa mkoani Kilimanjaro Februari 23, 2018.
Akwilina aliyefariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi akiwa kwenye daladala wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema
“Tutamuaga ndugu yetu siku ya Alhamisi katika viwanja vya chuo cha NIT pale Mabibo na siku hiyo hiyo tutaanza safari kuelekea Rombo-Mashati Olele mkoani Kilimanjaro na mazishi tutafanya Ijumaa,” amesema Kiyeyeu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni