Jumatatu, 12 Februari 2018

MEI 19 NI SIKU YA KUSEMA NDIYO:

Image may contain: people sitting




No automatic alt text available.


 Maandalizi ya harusi kati ya Prince Harry na Meghan Markle yameanza kwa kasi huku wawili hao wakitaraji kula kiapo chao mbele ya Askofu mkuu wa Kanisa la Canterbury, imefahamika kwa vyombo vya habari.
Wawili hao, wanataraji kufunga ndoa Mei 19, mwaka huu wakitaraji kutembea katikati ya makundi ya mashabiki wao litakaojitokeza kushuhudia wawili hao na dunia kwa jumla.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Kasri ya Kensington, msafara huo unataraji kupita katika mitaa sita kabla ya kuishia kwenye kasri la Windsor.
Ibada ya harusi hiyo, itafanyika kwenye kasri lililojengwa karne ya 15 la St George, na kuendeshwa na mkuu wa kanisa hilo la Windsor, Askofu David Conner.
Lakini baadaye wawili hao watakula viapo vyao mbele ya Askofu mkuu wa Canterbury, Justin Welby.
Harry, mwenye miaka 33, atakuwa wa kwanza kuruhusiwa kufungia ndoa ya kisasa kanisani licha ya kwamba anamuoa mwanamke aliyetalikiwa.

 Image may contain: 4 people, people smiling, people sitting and closeup

 Image may contain: 2 people, people standing

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni