Wakati Simba inajiandaa kuendeleza ubabe wake katika Ligi Kuu Bara, wapinzani wao, Mbao FC wanawaza mengine kabisa.
Simba
ndiyo vinara wa ligi hiyo na mechi yao ijayo ni dhidi ya Mbao FC kesho
Jumatatu. Lakini Mbao licha ya kuwa ugenini, wameapa kuwatuliza vinara
hao.
Mbao
wamesafiri kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kucheza na Simba mechi hiyo
ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, huku wakiwa na kumbukumbu ya
sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa awali.
Mwenyekiti
wa Mbao, Solly Njashi, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, kikosi chao
kipo kamili kwa ajili ya kukabiliana na Simba licha ya kwamba wapo
ugenini lakini wanataka pointi tatu tu.
"Sisi
tupo kamili kabisa kwa ajili ya mchezo wetu na Simba na tumekuja Dar es
Salaam kwa ajili ya kusaka pointi tatu, tumekuja kushangaza.
"Kocha
Etienne Ndayiragije pamoja na kikosi kizima kimejiandaa madhubuti
kabisa kwa ajili ya mchezo huo na tuna imani kwamba tutafanya vyema tena
baada ya kutolewa katika Kombe la FA," alisema Njashi.
Mbao
FC wanaamini wao hawashindwi kuwaangusha vigogo kwa kuwa katika mechi
ya kwanza ya msimu huu dhidi ya Yanga, Mbao waliifunga Yanga mabao 2-0
kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni