Bingwa mtetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga imepata mapokezi ya kutosha wakati wakiwasili Mtwara kwaajili ya mchezo wao dhidi ya Ndanda FC utakao pigwa katika dimba la Nangwanda hapo kesho siku ya Jumatano.
Video Player
00:00
01:00
Kikosi
cha Yanga kimefanya mazoezi ya mwisho hii leo kabla ya kuelekea katika
mchezo huo muhimu huku kocha mkuu wa timu hiyo Mzambia George Lwandamina
akisema kuwa timu yake ipo tayari kuivaa Ndanda FC.
Video Player
00:00
00:58
Kupitia kwa msemaji wa Yanga SC, Dismasi Ten amesema kuwa ameshakiandaa kikosi chake vizuri kwaajili ya kupata matokeo katika mchezo huo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kuweza kusonga mbele.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni