Mwanamasumbwi
raia wa Uingereza, Scott Westgarth amefariki dunia akiwa hospitali
baada ya kutwaa ubingwa wake dhidi ya Dec Spelman huko Doncaster.
Westgarth
mwenye umri wa miaka 31, alianguka katika chumba chake cha kubadilishia
nguo siku ya Jumamosi kufuatia kutwaa mkanda kwa pointi raundi ya 10
dhidi ya Spelman.
Kwa
upande wa promota wake, Stefy Bull kupitia mtandao wake wa Twitter
amesema kuwa “Nimemshuhudia kijana akifanya kazi anayoipenda kiasi
kwamba yupo tayari kuhatarisha hata maisha yake, sina maneno mengi ya
kusema hasa katika kipindi hiki kigumu kwa familia, timu na marafiki
hakika inauma,” amesema Bull.
Taarifa zinasema kuwa Westgarth ameonekana kuwa mwenye maumivu baada ya pambano hilo licha ya kuposti picha yake inayomuonyesha akisherehekea ushindi aliyo upata kabla ya kuanguka katika chumba cha kubadilishia nguo na kufikishwa hospitali ya Royal Hallamshire.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni