January 25, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba ametangaza rasmi kusimamisha zoezi la utoaji wa hati za kusafiria za jumla na kwa makundi mpaka pale watakapokuwa wameweka utaratibu wa kuendelea kufanya hivyo.
Dr. Mwigulu Nchemba
amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo na kusema
hatua hiyo imekuja baada ya kupokea taarifa ya mateso wanayoyapata
vijana wanaosafirishwa kutoka nchini Tanzania kwenda nje ya nchi kwa
kisingizo cha kufanyakazi tofauti tofauti.
“Nasimamisha
utoaji wa hati ya kusafiria ‘Passport’ za jumla za makundi za vijana
wanaokuwa wanapata mikasa hiyo ya kunyanyaswa, kutumikishwa, kuteswa
kikatili na wengine kuwekwa rehani kwa masuala ya dawa za kulevya”, -Dr. Mwigulu Nchemba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni