Kwenye muendelezo wa kupambana na ndoa za utotoni Tanzania leo January 24, 2018 Shirika la Msichana Initiative limezindua kitabu maalum kama njia ya kukomesha ndoa hizo ambazo zinahatarisha maisha na ustawi wa wasichana.
Katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo Rebeca Gyumi amewaeleza Waandishi wa Habari kuwa kitabu hicho kimebeba maudhui mbalimbali kuhusu ndoa za utotoni na jinsi ya kukabiliana nazo.
Gyumi amesema kitabu hicho kimeandikwa kwa lugha nyepesi na kiufupi ili iwe rahisi kueleweka ambapo ndani yake sehemu ya tafiti zinaonyesha kuwa Wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla ya kufikia umri wao.
Hiyo husababisha Wasichana hao kukumbwa na matatizo mengi wanapoingia katika ndoa hizo ikiwemo changamoto wakati wa kujifungua na kunyimwa haki ya msingi ya kupata elimu.
Pia Gyumi amesema katika utafiti wa mwaka 2016 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ilibainika kuwa wasichana wengi wanauelewa mdogo sana wa elimu ya afya ya uzazi “zaidi ya 50% ya wasichana wenye miaka 18 hawana uelewa huo kabisa” – Rebecca
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni