
KIKOSI cha Majimaji leo Jumatano kinatarajia kuingia jijini Dar ikiwa ni
muda mfupi kabla ya kuvaana na wapinzani wao Simba katika pambano la
ligi ambalo litapigwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa.
Majimaji wanaodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Sokabet,
inatua Dar ikiwa na kikosi kamili kwa ajili ya mchezo huo na Simba
ambapo mchezo wao wa mwisho waliilazimisha sare Singida United ya
kufungana bao 1-1.
Kocha msaidizi wa timu hiyo iliyo katika nafasi ya 12, Habibu Kondo
ameliambia Championi Jumatano, kuwa wamekuja Dar kuhakikisha
wanaendeleza mwendo wa kukusanya pointi kama walivyofanya kwenye
michezo yao miwili ya mwisho dhidi ya Azam na Singida United kabla ya
kuivaa Simba.
“Kesho (leo) Jumatano ndiyo tunatarajia kufika huko Dar kwa ajili ya
kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya kucheza na wenyeji wetu Simba,
tunawaheshimu wapinzani wetu kama timu kubwa lakini tunataka kufanya
vizuri mbele yao.
“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila tumejipanga vyema kwa ajili ya
kupata pointi mbele ya wenzetu hao, tunakuja tukiwa kamili kwa maana ya
kikosi chote na siku chache ambazo tutakaa huko zitatufanya kuzoea
mazingira kabla ya kupambana na wapinzani wetu,” alisema Kondo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni