Wanasayansi nchini Brazil wamegundua aina ya nyoka vipofu wenye umbo kama uume wa binadamu.
Tuwie radhi kama picha hizi zitakuondolea hamu ya kula lakini huu ni uumbaji wa Mungu.
Nyoka
hawa wa ajabu aina ya ‘atretochoana eiselti’ walipatikana kwenye bwawa
la kuzalisha umeme ambapo wakandarasi walikuwa wakifanya ukarabati
kwenye misitu ya Amazon.
Wana
baiolojia waliwapata nyoka hawa wenye umbo la ajabu sita wenye urefu
wa mita moja chini ya mto Madeira huko Rondonia, Brazil.
Nyoka
huyo anaweza akawa na muonekano usiopendeza lakini huu ni ugunduzi
unaovutia kwa wanayasansi wanaomini kuwa wanauhusiano na vyura.
Wanasayansi wamesema licha ya viumbe hao kuonekana kama nyoka lakini sio jamii ya reptilia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni