
Utafiti mpya uliofanywa na mtandao wa kijamii nchini China umeonesha kuwa hali ya usingizi wa wafanyakazi wa ofisini si nzuri, hasa wafanyakazi wanaopanga nyumba moja, ambao asilimia 20 kati yao wanalala baada ya saa saba usiku.
Utafiti huo umeonesha kuwa wafanyakazi wengi wanalala kati ya saa nne hadi sita usiku, na baadhi yao wanachelewa zaidi kulala.
Sababu kuu ya kuwachelewesha kulala ni matumizi ya mtandao wa Internet, kucheza game, kuchat na mambo mengine, tabia ya kuchelewa kulala na zamu za usiku.
Zaidi ya asilimia 55 ya wafanyakazi waliohojiwa wamesema, kutumia
mtandao wa kijamii, kusoma forum na kununua bidhaa kwenye mtandao wa
internet ni jambo la lazima kabla ya kulala.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni