Alhamisi, 4 Januari 2018

Treni yagonga lori na kushika moto Afrika Kusini

Image may contain: outdoor and nature







Takribani abiria 12 wamefariki dunia katika ajali ya treni ya abiria iliyoshika moto baada ya kugongana na lori na kisha kupinduka nchini Afrika Kusini.

Maafisa wa Afrika Kusini wasema watu wengine 268 wamejeruhiwa.
Polisi wamenukuliwa wakisema takribani abiria 850 wameondolewa kutoka kwenye treni hiyo wakiwa salama.


Scene of crash


Ukanda wa video umeonesha behewa moja la treni hiyo likiwa linawaka moja, pembeni kukiwa na gari lililopondwa pamoja na lori lililopinduka.
Abira ambao waliokolewa kwenye treni hiyo walikuwa pembeni na mizigo yao wakiwa wamekwama.
Ajali hiyo ilitokea karibu na mji wa Kroonstad katika jimbo la Free State baada ya lori kukosa kusimama katika makutano ya barabara na reli.

 Polisi wamenukuliwa wakisema abiria 850 wameondolewa kutoka kwenye treni hiyo wakiwa salama.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni