Ijumaa, 26 Januari 2018

Ruby ametangaza kuomba msamaha leo






Muimbaji wa Bongofleva Ruby baada ya kimya chake cha muda mrefu kwenye game ya Bongofleva kwa madai kutofautiana na watu kadhaa ikiwemo Ruge Mutahaba ambaye alikuwa anamsimamia kupitia kituo cha Tanzania House of Talent (THT) leo ameamua kuyamaliza.
Ruby leo alikuwa na interview katika kipindi cha XXL cha Clouds FM na amejibu maswali mengi ikiwemo kuomba msamaha kutokana na kumkosea Ruge Mutahaba na sasa anaanza upya, Ruby alikuwa kimya toka April 2017, hivyo kwa sasa anajiandaa kurudi na ataitambulisha management yake mpya.
 Nilihitaji kuwa na peace niliamua kuomba msamaha Ruge Mutahaba ni kama baba yangu, anaweza kuwa na mapungufu yake lakini sio mengi kuzidi wema wake, mimi na Nandy hatuna tatizo tunapendana na tunasapotiana”>>> Ruby
“THT pale ni nyumbani naenda pale muda wowote nafanya kazi zangu lakini kuhusu uongozi siwezi kuongelea chochote kwa sasa lakini mimi ni mtoto wa Clouds”>>>Ruby
CHANZO: Clouds FM
“Usijifanye jini kujua, wakati una silaha za nguvu za giza”-Ruby

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni