Ijumaa, 26 Januari 2018

Mjue Mwanafunzi wa primary mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani

Elimu haina mwisho haijalishi upo katika umri gani lakini wakati wowote na saa yoyote unaweza kuamua kwenda kuongeza elimu yako, moja kati ya stori niliyokutana nayo mtandaoni ni pamoja na hii ya bibi mwenye umri wa miaka 90 kurudi shule.

Priscilla Sitienei bibi mwenye umri wa miaka 90 lakini amechukua headlines sana nchini Kenya baada ya kuwa katika list ya wanafunzi wa Primary, Priscilla ambaye anatajwa kuwa ndio mwanafunzi umri mkubwa duniani kwa wanafunzi wanaosoma elimu ya msingi, kilichomsukuma kwenda shule ni hamu ya kutaka kujua kutumia simu na kutaka kujua kusoma maandiko ya Biblia.

Bibi Priscilla ambaye haoni aibu kujichanganya na wanafunzi wenzake ambapo ni sawa na wajukuu zake, anasoma katika shule ya msingi ya Leaders Vision iliyopo Eldoret nchini Kenya, hata hivyo uamuzi wa Bibi huyo umefanya apokee pongezi kutoka sehemu mbalimbali.






chanzo na millardayo blog.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni