Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amefikisha mabao 10 na kuamsha mbio za ufungaji mabao.
Awali Okwi alikwama akiwa na mabao nane kwa kipindi kirefu hadi mshambuliaji wa Mbao FC, Habibu Kiyombo akafikisha mabao saba.
Lakini leo Okwi amefunga mabao mawili
wakati Simba ikiimaliza Singida United kwa mabao 4-0 katika mechi ya
Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni