
enyekiti wa Kamtai ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ametoa zawadi ya gari kwa mchezaji wa Simba, Said Hamis Ndemla.
Hans Poppe ametangza kumpa Ndemla gari baada ya kuonyesha kiwango kizuri cha kuvutia katika mechi dhidi ya Singida United, leo.
Simba
imeshinda kwa mabao 4-0 katika mechi hiyo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu
kubwa na mashabiki wa soka nchini. Ndemla alitengeneza mabao mawili moja
akifunga Emmanuel Okwi na jingine Asante Kwasi.
Akizungumza
na hivi punde, Hans Poppe amesema mechi ya leo imekuwa ni
fainali ya uamuzi wake lakini amekuwa akimfuatilia Ndemla.
“Nilikuwa
nikimfuatilia kama ambavyo nimekuwa nikisema nahitaji mchezaji mwenye
nidhamu na ambaye hawezi kubadilika. Utaona Ndemla amekuwa benchi lakini
akiingia uwanjani anaonyesha mchango wake,” alisema.
“Tena
pamoja na kukaa benchi, hakuwahi kuonyesha utovu wa nidhamu. Badala
yake kila akipata nafasi amekuwa akijituma na kuisaidia timu.”
Hii
ni mara ya pili Hans Poppe anatoa gari kwa mchezaji wa Simba. Alianza
na Hussein Zimbwe aliyempa gari aina ya Toyota Raum. Lakini akaonyesha
gari aina ya Toyota Lactic na kusema atapewa mchezaji atakayefanya
vizuri.
Kuhusiana na aina, leo amesema: “Aina utaijua baadaye ila gari haiko mbali. Hivyo tutaangalia siku yenye nafasi atakabidhiwa.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni