Ijumaa, 26 Januari 2018

Nikki wa Pili amjibu Joshua Nassari



 ba si kweli kuwa wameamua kumtumikia 'kafiri' ila kimsingi wao hawana ufahamu wa kuongelea masuala ambayo bado yanaendelea Kimahakama.

Nikki amebainisha hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hii baada ya Mbunge huyo kutoa lawama zake kwa wasanii katika ukurasa wake wa twitter asubuhi ya leo kutokana na kuwaona wapo kimya katika kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi 'Sugu' ya kutoa maneno yenye kuleta chuki kati ya serikali na wananchi wakati alipokuwa katika mkutano wake wa hadhra ambao ulifanyika Disemba 31, 2017 jijini Mbeya.

Huu hapa chini ndio ujumbe wenyewe wa Mhe. Joshua Nassari



"Wasanii hawana umoja, chama chao hakina nguvu kwa hiyo hata kunapotokea jambo wasanii walitolee sauti kwa pamoja kuna hakuna 'platform' ya kushikilia jambo hilo na kujikuta kila msanii yupo peke yake, na kupaza sauti kila mtu peke yake wasanii wengi wanaogopa hilo", alisema Nikki wa Pili.

Pamoja na hayo, Nikki wa Pili aliendelea kwa kusema si jambo la kweli kama watu wanavyodhania kuwa tasnia ya muziki imemtenga Sugu ila tatizo lipo katika namna ya uwasilishaji wa jambo hilo.

"Hapana hatuwezi kumtenga Mhe. Sugu ila kuna jambo moja naweza kusema kwamba hili suala bado lipo kimahakama na tumeona wenyewe wamewaweka Wanasheria, kwa hiyo sisi wasanii bado hatuna ufahamu wa kujua jambo likiwa Mahakamani unaweza kulisema kwa upande gani kwa maana mara nyingi huwa tunaambiwa tusiingilie kazi za Mahakama", alisisitiza Nikki wa Pili.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni