Watoto
waRohingya katika kambi ya Chonkhola huko Chakdhala, Bangladesh ambapo
kumezuka kwa diphtheria. © UNHCR / Andrew McConnell
Makubaliano ya serikali hizo mbili yanazitaka zihakikishe kuwa wakimbizi hao sio tu wanarejea kwa hiari lakini pia kwa usalama vijijini kwao nchini Myanmar.
Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards amesema hadi sasa hakuna hakikisho kwa wakimbizi hao kurejea salama na kwa hiari na hivyo kuitolea wito serikali ya Myanmar
Kwa mara nyingine tena tunaitolea wito serikali ya Mynamar iruhusu ufikishaji wa huduma za kibinadamu kwenye jimbo la Rakhine bila masharti yoyote na pia kuweka hali halisi za kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo"
Aidha amesema kuwa wakimbizi wengine wanaendelea kuwasili nchini Bangladesh wakitoka jimbo la Rakhine.
Akisisitiza mchakato wa wakimbizi kuweza kuchukua uamuzi wa kurejea kwa hiari ni sharti vigezo kadhaa viwepo akitoa mfano.
" Wakimbizi wanahitaji kufahamishwa kupitia njia muafaka na pia kushauriwa kuhusu hali yenyewe ili kurejea kwao kuweze kuwa salama, kwa hiari na kuwe endelevu."
Amesema UNHCR iko tayari kuendelea kushirikiana na serikali zote ili kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo kwa manufaa ya pande zote husika ikiwemo jamii za jimbo la Rakhine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni