
Mwananfunzi Aghata Mwananyau (19), aliyekatisha masomo akiwa kidato cha
nne baada ya kupewa ujauzito, amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela au
kulipa faini ya shilingi 300,000.
Msichana huyo aliyekuwa akisoma katika Shule ya Sekondari ,kangale,
katika Mji wa Namanyere, wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa, aliacha masomo
baada ya kupewa ujauzito na Alfa Nestory (20).
Mshtakiwa huyo alishindwa kulipa faini hiyo ambapo ameanza kutumikia adhabu hiyo.
Juzi aliitwa na upande wa mashtaka kutoa ushahidi katika Mahakama ya
Wilaya ya Nkasi, mbele ya Hakimu Ramadhani Rugemalira ambapo alitoa
ushahidi wa uongo akisema aliyempatia ujauzito hakuwa mshtakiwa Nestory
bali alikuwa ‘mmachinga’ aliyetokea Mbeya, tofauti na maelezo ya awali.
Ndipo Mwendesha Mashtaka, Hakimu Gwelo, alipomshtaki kwa kutoa ushahidi
wa uongo, ambapo jana alifikishwa mahakamani hapo na alisomewa mashtaka
hayo, na alikiri kutenda kosa hilo.
Akitoa hukumu, Hakimu Rugemalira, alisema amezingatia utetezi wa
mshtakiwa kuwa apunguziwe adhabu kwa kuwa ana mtoto mchanga mwenye umri
wa miezi nane.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni