Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye yuko nchini
Uswisi kushiriki Mkutano wa Baraza la uchumi Duniani huko Davos,
amekaribisha wawekezaji wa nchi za nje nchini Zimbabwe, kwa lengo la
kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.
Rais Mnangagwa
amesisitiza kuwa Zimbabwe iko wazi kwa nchi zote za kigeni na jukumu kuu
kwa serikali ni kufufua uchumi, na kuahidi kupunguza vizuizi kwa
wawekezaji kutoka nchi hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni