mwana wa liganga blog ni blog ya kutoa taarifa, matukio, yaliyotokea katika ulimwengu hususani katika nchi yaTanzania blog hii inasimamiwa na mwandishi wa habari kitaaluma bwana Deus Thomas liganga.lengo ni kutoa taarifa kwa umma,kwa maendeleo ya taifa na Dunia kwa ujumla kwa mawasiliano kuhusu mtangazo, habari, wasiliana nasi 0659944423,deusliganga@yahoo.com,mzeeliganga@gmail.com
Jumatatu, 22 Januari 2018
Makumbusho ya Taifa yamzungumzia binadamu wa kwanza
Makumbusho ya taifa la Tanzania iliyopo jijini Dar es salaam imeandaa mafunzo ya onesho la chimbuko la binadamu Afrika yanayotarajiwa kutolewa kesho.
Mkurugenzi wa Makumbusho ya taifa Prof. Audax Mabula mafunzo na onesho hilo yanatokana na tafiti mbalimbali zinazofanyika bonde la hifadhi ya Olduvai na Laetol katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro.
Aidha Prof. Audax ameeleza onesho hilo litafanyika kesho jijini Dar es salaam na litafunguliwa na waziri wa Mali asili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na litahudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Katika onesho hilo wananchi pia wataweza kuona mambo mbalimbali ya kale ambayo binadamu wa kwanza aliweza kuyafanya katika nyanja tofauti katika maisha yake.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni